Friday, October 14, 2011
Ingawa kila siku idadi ya bloggers wa kitanzania inazidi kuongezeka,idadi ya wanawake wanaoblog bado ni ndogo ikilinganishwa na wale wa kiume.Yawezekana ni kwa sababu wanawake bado hawajapata mwamko wa kutosha au pengine ni kitu ambacho bado wanakipa kisogo. Lakini pamoja na idadi ya wanawake kuwa ndogo,wanaofanya hivyo wanafanya kazi nzuri sana ya kuwawakilisha wanawake wenzao.Miongoni mwa wanawake hao ni pamoja na Shamim Mwasha au Zeze kama anavyojulikana kwa watu wake wa karibu. Iwe ni shughuli yenye mvuto wa kitaifa au wa mtu binafsi(hususani zile zenye kuwagusa wanawake zaidi),ukihudhuria na kutizamatizama katika watu waliopo mstari wa mbele katika kuchukua kumbukumbu iwe ni kwa kutumia picha za mgando(still photos) au videos,bila shaka waweza kumuona Zeze.Ukimsalimia atakujibu na kukurushia tabasamu ambalo naweza kusema ni “signature” yake. Hivi karibuni nilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde.Zeze ambaye blog yake inakwenda kwa jina www.8020fashions.blogspot.com, anaweka bayana mambo kadhaa kuhusu harakati zake kama mwandishi wa habari(taaluma yake) na pia blogger pamoja na ujasiriamali. Yote tisa,kumi ni kwamba siku chache zijazo,Shamim kupitia blog yake ya 8020fashions,anasheherekea miaka mitano(5) tangu aanze shughuli ya kublog au Libeneke la kublog kama ambavyo rafiki yangu Issa Michuzi hupenda kuiita shughuli hii.Nimemuuliza pia maswali machache kuhusu siku hiyo maalum kwake na kwa wapenzi wa blog yake ambayo itafanyika pale Diamond Jubilee tarehe 30 October,2011.Twende pamoja katika mahojiano yafuatayo; BC: Umekuwa uki-blog kwa muda gani mpaka hivi sasa?Nini kilikusukuma katika kuanzisha blog yako? SM: Huu ni mwaka wangu wa tano sasa tangu nianze hili libeneke.Kikubwa kilichonisukuma kilikuwa ni nia yangu ya kutangaza biashara ya duka langu la nguo liitwalo 8020 Fashion lililopo Sinza.Nikaona nifungue blog ili niwe naweka nguo na bidhaa zingine kadiri zinavyowasili dukani.Sasa kama ujuavyo si kila siku naweza kuwa na new arrival na ili watu warejee kuangalia blog ndio nikaanza kuweka picha za matukio mbalimbali huku nikiwa nimejikita kwenye fashion zaidi katika kuonyesha nini kilivaliwa wapi na nani na mambo kama hayo. BC: Kitaaluma wewe ni mwandishi wa habari. Sasa ukiwa kama blogger,unadhani kuna tofauti gani za kimsingi kati ya mwandishi wa habari wa kawaida na blogger? Je,kuna misingi ambayo wote (a journalist and a blogger) wanayotakiwa kuzingatia? SM: Ni kweli kabisa,ipo tofauti kubwa sana. Kama ujuavyo blogger inakuwa ni mimi kama mimi ambapo nisipo-update ni blog inakuwa imelala doro. Hivyo kuwa kama blogger inabidi uwe na juhudi binafsi za kujituma kitu ambacho ni tofauti na mwandishi wa habari ambapo hata wewe usipoenda kazini au kufanya kazi gazeti ni lazima litoke tu. BC: Blog yako imejikita zaidi katika kuandika habari za urembo,shughuli kama vile harusi,kitchen party,fashion shows nk.Ni kwanini uliamua kuwa na “niche” kama hiyo? 


 Read more: BongoCelebrity

0 comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Blog Archive

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS