Friday, October 21, 2011
Pichani ni Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel,akipunga mkono wa kwaheri kwa baadhi ya ndugu,jamaa,marafiki na watanzania waliojitokeza kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) jijini Dar-es-salaam hapo jana. Salha ameondoka kwenda kushiriki katika mashindano ya dunia (Miss World) yatakayofanyikia jijini London nchini Uingereza mwezi ujao tarehe 6 Novemba katika ukumbi wa Earls Court Two ambapo mshindi wa Miss World 2010,Mmarekani Alexandria Mills atakabidhi taji lake kwa mshindi mpya. Swali kubwa ambalo najiuliza na ningependa nawe msomaji ujiulize ni kwamba je,mwaka huu Tanzania ina matumaini ya kufanya vizuri zaidi kuliko miaka ya nyuma?Tumefanya maandalizi ya kutosha ili kwenda kushindana na sio kushiriki katika mashindano haya?Na endapo tutaishia kuwa wasindikizaji,mwakani tujiandae namna gani?Tuwapate vipi wanaokwenda kutuwakilisha? Bila shaka majibu ya baadhi ya maswali hayo magumu yapo mikononi mwa Kamati ya Miss Tanzania.Kwetu sisi hapa BC,tunamtakia Salha kila la kheri.

 Read more: BongoCelebrity

0 comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Blog Archive

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS