Friday, June 22, 2012
Mwanamuziki wa Tanzania aliyetamba na vibao kama ‘Kwaaajili Yako’ na ‘Full Shangwe’ Hussein Machozi, amesema anafikiria kuhamia kabisa Kenya kwakuwa anahisi muziki wake unathaminiwa zaidi huko kuliko nyumbani. Akijibu swali la Bongo5 lililotaka kufahamu kama ana mpango huo kwakuwa ni muda mrefu sana sasa amekuwa akiutumia nchini Kenya kuliko Tanzania, Machozi alisema,”Yap naona pananifaa sana kwa muziki wangu ambao hauna unafiki si unajua watu wa huku sio wanafiki.” Kwanini anasema Tanzania kuna unafiki? “Okay, watu wa media hawako free kabisa yaani huwa wanafuata upepo wanapoanzisha wale wenye nguvu. Yaani wakitaka kumtoa mtu wao na media zingine zinafuata wala hawashtuki kuwa analazimishwa atoke, wakati kuna ngoma kibao kali wanazipotezea ili mtu wao apite. Matokeo yake wanatoaga ngoma moja inahit baada ya hapo ni pumba tupu. Huwa inaniuma sana.” “Kwa kenya mambo hayo hakunaga asee! Huku kama ngoma ni kali basi itatandikwa hadi noma, ila kama ni mbaya huwezi hata kuiskia. Nakubalika huku coz ngoma zangu ni kali na zina kichwa na miguu namaanisha wimbo uko na story ya kufuatilia na inaskilizika na rika zote, nadhani hii ni sababu tosha sana,” alisema Machozi. Msanii huyo tayari ameshafanya ngoma na wasanii wa Kenya wakiwemo Habida,Size 8 na DNA.
                          Picha zaidi ingia hapa http://millardayo.com/

              Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi.

           Janja amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.

           Amesema amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.

           kwenye sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati” Kwa kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi nawalaza chali matembo”

           Dogo Janja atasikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kuanzia saa moja leo usiku utapata nafasi ya kusikia alichosema na jinsi alivyopokelewa kwa shangwe.
Saturday, June 16, 2012
Monday, May 7, 2012

Sunday, May 6, 2012

Wednesday, April 18, 2012
Tuesday, April 17, 2012
Thursday, April 12, 2012
Wednesday, March 21, 2012
Saturday, March 10, 2012
WAS HAPPY MEETING WEMA THIS DAY AGAIN AS AM HER OFFICIAL MANAGER, THEN WE MOVED TO FITTING AND SHOOTING FOR MY NEW CLOTHING LINE CAMPAIGN.. NAPENDA PICAHSO BEFORE KAZI TULIPIGA PICHA KUHAKIKISHA MWANGA UKO SAWA..


HATUA YA PILI IKAFUATA KUCHAGUA MOJA YA MAKOTI NINAYOYATENGENEZA ILI KUPATA MOJA LINALOMFAA KULINGANA NA KAMPAINI NINAYOIFANYA KABLA MODELS WENGINE HAWAJAFIKA...

NA HILI NDIO BANGO (TANGAZO)LA MWEZI HUU KWA CAMPAIGN YA HII DESIGNS YA MAKOTI NINAYOYATENGENZA KWA SASA... JIPATIE LAKO KWA AJILI YA MSIMU HUU WA KUPENDEZA(KILIMANJARO MUSIC AWARDS SI UNAJUA SWALA LA RED CARPET PALE KATI....) NA SINGLE BUTTONS BLAZER
Monday, March 5, 2012
Track Mpya Ya Jaffarai ft Nazizi - Tembea Na Mimi ambayo imefanywa chini ya Prod Lamar na Dunga. 


MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa anafanya kazi hiyo nchini Kenya Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kuwa anafurahia kuishi nchini humo kwani anafanya muziki kwa raha bila karaha kama bongo.

 Akifanya mahojiano maalumu na DarTalk kwa njia ya mtandao wa kijamii wa facebook, Ray C, alidai kuwa tangu alipofika nchini humo amekuwa akifanya mambo yake kwa umakini mkubwa kuliko alipokuwa Tanzania.

Ray C katika pose

 Alisema kuwa hata hivyo kitu ambacho kinamsukuma endelea kuishi nchini humo ni kutokana na nafasi aliyonayo ya kuweza kujitangaza kimataifa kwani ni nchini ambayo wasanii wake wanafanya muziki unaendana na soko la kimataifa.

 “Muziki wa Kenya huwezi kuufananisha na Tanzania hata wasanii wa huku wako juu sana na wanafanya kazi siyo kutupiana majungu kama baadhi ya wasanii wa Tanzania,” alisema.

 Hata hivyo alipoulizwa ni lini atarudi nchini, alijibu “Dah sifikili kuja Tanzania kwa sasa kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya ambayo yanahitaji nitulie kweli ili huko ni nyumbani nitakuja tu,”.
Thursday, March 1, 2012


JAMANI NATAFUTA BINTI ATAKAE WEZA KUCHEZA NAFASI YA GUBE GUBE UKITAKA KUSHIRIKI KATIKA SHINDANO HILO PIGA NAMBA +255 715 973697 UTAPATA MAELEZO YOTE..........!!!!!
Friday, January 13, 2012


DARASA FT GODZILLA & JOH MAKINI – SIKATI TAMAA REMIX
Wednesday, January 11, 2012
Wimbo huu nimeupokea siku kadhaa zilizopita.Muda wa kuusikiliza kwa makini nao ukawa haba.Mambo ya mwanzo wa mwaka,kurudi kazini,watoto kurudi shuleni(gharama zake sasa!).Duh,elimu imekuwa bidhaa ya ghali sana.Sijui nichague elimu mtaani?

 Lakini kingine kilichonifanya “niskute” kidogo(niskute neno la zamani hili kiasi,enzi hizo) ni mabadiliko yaliyopo katika wimbo na msanii huyu.Ni kweli kwamba huyu ni Ferouz,yule yule alipitia enzi za kundi maarufu la Daz Nundaz.Ni kipaji au kujaribu soko.Ni kuingia au kutoka.Ni risk.Good or bad.Inategemea na maoni yako wewe msikilizaji.

 Msikilize Ferouz katika wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina Majoto ukiwa katika style ya mchiriku,maarufu kutoka jijini Dar na pembezoni aka Pwani.Nini maoni yako?Kaelekea kuliko au kachemsha?

- Song – Majoto
- Artist – Ferouz
- Producer
– Pancho Latino
- Studio – B Hit’z
























Msanii Diamond na wacheza show wake wakiwa mahakama ya Mwanzo Iringa
 kusubiri hukumu (picha na Misanjo Liviga Mlalah. 
Na Misanjo Livinga Mlalahoi Iringa 
MAMIA wafurika kushuhudia hukumu ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul a.k.a Diamond akihukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya shilingi elfu 50.000 kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari mkoani Iringa Francis Godwin 
Hatua hiyo imekuja baada ya msanii Diamond na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya mahakama yeye na wenzake kwa kuharibu Camera 
mbili, Lap top aina ya Accer pamoja na kumshambulia mwanahabari Francis Godwin Desemba 31 mwaka jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa. 
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Hakimu Masua alisema kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu kwenda jela miezi 6 au kulipa fidia ya shilingi elfu hamsini kila mmoja na huku wakilazimika kumlipa Godwin shilingi elfu 30 kila mmoja na kufanya kufikia kiasi cha shilingi 90000 Wakitoa utetezi wao watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia adhabu kwa kuwa hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja mkoani hapa kwa ajili ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo wamelifanya kwa ghadhabu. Mheshimiwa Hakimu ninaomba unipunguzie adhabu licha ya kutenda kosa hilo, kwani nakili kuwa nilipatwa na hasira kama binadamu na kuamua kuchukua uamuzi wa kufanya hayo, mimi sikukusudia kuja Iringa kufanya vurugu bali hali hiyo ilikuja baada ya kupata ghadhabu kama walivyo binadamu wengine,” alisema Diamond. Naye mwanasheria Evaristo Myovela alisema kesi hiyo hakimu ametimiza wajibu wake, huku akimshauri Francis kukata rufaa kama hajaridhika na maamuzi ili kuipeleka kesi hiyo katika Mahakama nyingine kwa kufuata utaratibu wa sheria katika kuchukua maamuzi hayo. Wakati wanahabari wakijadili juu ya hukumu ya Diamond , mara Waziri wa sera na uratibu wa sheria za bunge Willium Lukuvi alikatiza katika mahakama hiyo ndipo wanahabari wakataka kupata mawazo na uelewa zaidi juu ya hukumu hiyo. Hata hivyo Diamond alilipa fidia hiyo na kuachiwa huru licha ya Godwin kuamua kupeleka barua mahakamani ya kuomba nakala ya kesi na 13. ya 2012 kwa ajili ya kukata rufaa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS