Friday, January 13, 2012


DARASA FT GODZILLA & JOH MAKINI – SIKATI TAMAA REMIX
Wednesday, January 11, 2012
Wimbo huu nimeupokea siku kadhaa zilizopita.Muda wa kuusikiliza kwa makini nao ukawa haba.Mambo ya mwanzo wa mwaka,kurudi kazini,watoto kurudi shuleni(gharama zake sasa!).Duh,elimu imekuwa bidhaa ya ghali sana.Sijui nichague elimu mtaani?

 Lakini kingine kilichonifanya “niskute” kidogo(niskute neno la zamani hili kiasi,enzi hizo) ni mabadiliko yaliyopo katika wimbo na msanii huyu.Ni kweli kwamba huyu ni Ferouz,yule yule alipitia enzi za kundi maarufu la Daz Nundaz.Ni kipaji au kujaribu soko.Ni kuingia au kutoka.Ni risk.Good or bad.Inategemea na maoni yako wewe msikilizaji.

 Msikilize Ferouz katika wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina Majoto ukiwa katika style ya mchiriku,maarufu kutoka jijini Dar na pembezoni aka Pwani.Nini maoni yako?Kaelekea kuliko au kachemsha?

- Song – Majoto
- Artist – Ferouz
- Producer
– Pancho Latino
- Studio – B Hit’z
























Msanii Diamond na wacheza show wake wakiwa mahakama ya Mwanzo Iringa
 kusubiri hukumu (picha na Misanjo Liviga Mlalah. 
Na Misanjo Livinga Mlalahoi Iringa 
MAMIA wafurika kushuhudia hukumu ya msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul a.k.a Diamond akihukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya shilingi elfu 50.000 kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari mkoani Iringa Francis Godwin 
Hatua hiyo imekuja baada ya msanii Diamond na wacheza shoo wake wawili kukiri kosa mbele ya mahakama yeye na wenzake kwa kuharibu Camera 
mbili, Lap top aina ya Accer pamoja na kumshambulia mwanahabari Francis Godwin Desemba 31 mwaka jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa. 
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Hakimu Masua alisema kulingana na watuhumiwa wote watatu kukiri kosa hilo anawahukumu kwenda jela miezi 6 au kulipa fidia ya shilingi elfu hamsini kila mmoja na huku wakilazimika kumlipa Godwin shilingi elfu 30 kila mmoja na kufanya kufikia kiasi cha shilingi 90000 Wakitoa utetezi wao watuhumiwa hao walisema mahakama iwapunguzia adhabu kwa kuwa hawakukusudia kufanya kosa hilo, na wao walikuja mkoani hapa kwa ajili ya kutoa burudani, na kuwa tukio hilo wamelifanya kwa ghadhabu. Mheshimiwa Hakimu ninaomba unipunguzie adhabu licha ya kutenda kosa hilo, kwani nakili kuwa nilipatwa na hasira kama binadamu na kuamua kuchukua uamuzi wa kufanya hayo, mimi sikukusudia kuja Iringa kufanya vurugu bali hali hiyo ilikuja baada ya kupata ghadhabu kama walivyo binadamu wengine,” alisema Diamond. Naye mwanasheria Evaristo Myovela alisema kesi hiyo hakimu ametimiza wajibu wake, huku akimshauri Francis kukata rufaa kama hajaridhika na maamuzi ili kuipeleka kesi hiyo katika Mahakama nyingine kwa kufuata utaratibu wa sheria katika kuchukua maamuzi hayo. Wakati wanahabari wakijadili juu ya hukumu ya Diamond , mara Waziri wa sera na uratibu wa sheria za bunge Willium Lukuvi alikatiza katika mahakama hiyo ndipo wanahabari wakataka kupata mawazo na uelewa zaidi juu ya hukumu hiyo. Hata hivyo Diamond alilipa fidia hiyo na kuachiwa huru licha ya Godwin kuamua kupeleka barua mahakamani ya kuomba nakala ya kesi na 13. ya 2012 kwa ajili ya kukata rufaa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS