Saturday, November 19, 2011
Bila shaka yaelekea huu ni msimu mpya wa ngoma mpya kuachiwa.Kila msanii anataka kufurahia mwisho wa mwaka akiwa ameachia kitu kipya hewani.Huenda hiyo ndio zawadi ya Xmas kwa mashabiki. 

Mambo kadhaa yamemtokea Marlaw mwaka huu.Kikubwa zaidi ni kwamba hivi sasa ni mume wa mtu.Utakumbuka kwamba yeye na msanii mwingine,Besta,walifunga ndoa mwaka huu katika mojawapo ya harusi ambazo ziligubikwa na usiri mkubwa hususani kwa upande wa vyombo vya habari.Baada ya ndoa akawa kimya kidogo katika masuala ya muziki hususani kwa upande wa kutoa vibao vipya ingawa amekuwa akionekana majukwaani hususani katika shughuli mbalimbali zinazohusu Chama Cha Mapinduzi.Marlaw ni mtu asiyeficha mapenzi yake kwa chama tawala. 

Sasa baada ya kutamba na vibao kadhaa kikiwemo kile cha Pii,Pii(Missing My Baby),msanii Marlaw(ukipenda unaweza kumuita mume wa Besta) ameachia kibao Mbayuwayu(Ngo ngo ngo).Bila shaka hii itakuwa ni another sing-a-along kutoka kwa Marlaw.Ni utabiri wangu wa haraka haraka.Wimbo huu umetengenezwa pale Fishcrab chini ya Producers Lamar,Tud Thomas na Dunga.Usikilize hapo chini Read more: BongoCelebrity

0 comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Blog Archive

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS