Saturday, December 3, 2011
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Sam Wa Ukweli, anashukuru management mpya ya Aljazeera Entertainment kwa kusimamia kazi zake kwa sasa,ambayo hapo awali ilikuwa inasimamia kazi za Diamond. Akiongea na DarTalk Sam alisema ‘’Ninamshukuru Mungu kwa kuwa chini ya Menejimenti ya Aljazeera Entertainment, natarajia kuachia albam yangu ya pili hivi karibuni ambayo ndani yake kutakua na wasanii wakali ambao wananipa sapoti, kama vile Linex, Barnaba, Linah, Kidumu kutoka kenya pamoja na wasanii wengine kibao’’. Vilevile aliendelea kusema anatarajia kuachia nyimbo mbili kila mwaka ambazo ni kali, hivyo anaomba mashabiki wake kukaa tayari kwa kuipokea albam hiyo pamoja na video. Msanii huyo anatamba na nyimbo zake kali kutoka kwenye albam yake ya kwanza ambazo ni ‘Sina raha’ pamoja na ‘Hata kwetu wapo’, nyimbo zilimtambulisha vizuri kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya.

0 comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS