Friday, June 22, 2012
Mwanamuziki wa Tanzania aliyetamba na vibao kama ‘Kwaaajili Yako’ na ‘Full Shangwe’ Hussein Machozi, amesema anafikiria kuhamia kabisa Kenya kwakuwa anahisi muziki wake unathaminiwa zaidi huko kuliko nyumbani. Akijibu swali la Bongo5 lililotaka kufahamu kama ana mpango huo kwakuwa ni muda mrefu sana sasa amekuwa akiutumia nchini Kenya kuliko Tanzania, Machozi alisema,”Yap naona pananifaa sana kwa muziki wangu ambao hauna unafiki si unajua watu wa huku sio wanafiki.” Kwanini anasema Tanzania kuna unafiki? “Okay, watu wa media hawako free kabisa yaani huwa wanafuata upepo wanapoanzisha wale wenye nguvu. Yaani wakitaka kumtoa mtu wao na media zingine zinafuata wala hawashtuki kuwa analazimishwa atoke, wakati kuna ngoma kibao kali wanazipotezea ili mtu wao apite. Matokeo yake wanatoaga ngoma moja inahit baada ya hapo ni pumba tupu. Huwa inaniuma sana.” “Kwa kenya mambo hayo hakunaga asee! Huku kama ngoma ni kali basi itatandikwa hadi noma, ila kama ni mbaya huwezi hata kuiskia. Nakubalika huku coz ngoma zangu ni kali na zina kichwa na miguu namaanisha wimbo uko na story ya kufuatilia na inaskilizika na rika zote, nadhani hii ni sababu tosha sana,” alisema Machozi. Msanii huyo tayari ameshafanya ngoma na wasanii wa Kenya wakiwemo Habida,Size 8 na DNA.
                          Picha zaidi ingia hapa http://millardayo.com/

              Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi.

           Janja amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza.

           Amesema amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa.

           kwenye sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati” Kwa kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi nawalaza chali matembo”

           Dogo Janja atasikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kuanzia saa moja leo usiku utapata nafasi ya kusikia alichosema na jinsi alivyopokelewa kwa shangwe.
Saturday, June 16, 2012

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS