Monday, November 28, 2011
Na Mwandishi wetu

 Hatimaye lile tamasha lililokuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa la Street University linafanyika leo (Jumapili) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo akiwemo Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa ‘20%’, Glorious Singers, Dot Com Generation na wengine wengi watamfungulia pazia mjasiriamali wa kimataifa na mzungumzaji wa kutia hamasa (motivational speaker), Eric Shigongo atakayekuwa mtoa mada kwenye tamasha hilo.

 Shigongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Global Publishers and General Enterprises, atafundisha namna ya kupata wazo la kibiashara, jinsi ya kukuza mitaji, kupata mikopo benki, kujikwamua kimaisha kupitia ujasiriamali na mada nyingine nyingi sambamba na mtoa mada mwenzake, James Mwang’amba kwenye tamasha hilo litakaloanza saa tano asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.

 Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, James Mwang’amba tiketi zinapatikana Arusha kwenye Supamaketi ya Shoprite, Summit Centre, Cordial Tours, Hoteli ya Acquiline, Kasi Store, Hoteli ya Kibo Palace na uwanjani (Sheikh Amri Abeid) kwa shilingi elfu tano tu.

 Wadhamini wa tamasha hilo ni Kampuni ya Global Publishers Ltd, Malta Guinness, Airtel, Azania Bank, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Wauzaji na wasambazaji wa vipodozi asili wa Oriflame, Hoteli ya Corridor Springs ya Arusha, Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA) na Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha.

 Wadhamini wengine ni Tripple A Radio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM), Radio 5 (105.7FM) na Sauti ya Injili Radio (92.2/96.2 FM) zote za jijini Arusha.
Saturday, November 26, 2011
Miezi kadhaa nyuma niliwahi kuuliza swali kuhusu nani aliye zaidi katika ya Steven Kanumba na Ray Kigosi.Mashabiki na wafuatiliaji wa Bongo Movies mkatoa ushirikiano mkubwa na kueleza bayana yule ambaye mnadhani ni zaidi ya mwenzake.Mpaka leo hii bado comments kuhusu hoja ile bado zinaendelea.Hiyo,kwa upande mwingine,inaonyesha ni kwa jinsi gani watu zaidi wanafuatilia sanaa ya filamu nchini Tanzania.Ni jambo zuri.

 Leo naomba tuhamie kidogo upande wa waigizaji wa kike kwani ni wazi kabisa na wao wanafanya vizuri sana katika kuendeleza fani hii ambayo kwa miongo kadhaa ilipewa kisogo.Mchango wao ni dhahiri.Hapa naomba niwaweke “kikaangoni” Monalisa (Yvonne Cherryl) na Blandina Chagula maarufu kama Johari. Bila shaka umeshawahi kuwaona katika uigizaji wa aina mbalimbali.Endapo ungekuwa na filamu yako na ukawa unatafuta mwigizaji wa kike(lead actress) ungemchagua nani katika ya Monalisa au Johari.Kwa ufupi unadhani nani zaidi kati yao?Kwanini?



                                             Johari

                                 MONALISA
Sina uhakika unaisomea wapi habari hii lakini nahisi unaisomea ukiwa katika mitkasi yako ya kila siku iwe ni kazini au katika sehemu zinginezo za kutafutia riziki.Kwa ufupi unafanya kitu! Lakini je,umeshawahi kuketi chini na kujiuliza kwa undani kabisa kwamba kwanini unafanya unachokifanya? Nini kinakusukuma kufanya hivyo?Unapohisi kukata tamaa na kitu unachokifanya,kwanini unaendelea? Maudhui kama hayo hapo juu ndio yaliyomo katika wimbo mpya wa Mike Tee(Mnyalu) ambao amemshirikisha Fareed Kubanda au ukipenda Fid Q. Wimbo unazungumzia zaidi sanaa ya muziki.Ni wangapi wanafanya muziki kwa sababu wanapenda au wengi wanafanya kwa “Sababu Ya Njaa”?Msikilize kwa makini Mike Tee hapa.
Kutoka pande za Temeke,Wanaume TMK wanaingiza karata yao.Wimbo unaitwa “Kichwa Kinauma“. Umetengenezwa pale Masaki kwa MJ Records chini ya Producer Marco Chali(Doctor Chali). Read more: 
Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama. wa kwanza( kulia) wakiwanyumba ya jukwa na mwana muzingi aliekuwa anasubiriwa kwa hamu siku ya jana Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving Muimba Jose Chameleone katikatia, akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wake
Cheza nikucheze juu na chini warembo wa Kiganda ndani ya Nyumba
Mamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.
Cheif wa swahilivilla Abou Shatry akipata picha ya pamoja na kundi zima la muimbaji kutoka Uganda Jose Chameleone.
Aj Ubao alikuwa ni mumbaji wa pili kuimba katika onyesho hilo waliosherikiana na mwanamuziki wa kutoka Uganda Jose Chameleone, wakiwa nyuma ya jukwa akipata flash ya pamoja na mdhamin wake wapendo
Muimbaji Ana Lov akipata flash ya pamoja na rafiki yake kwenye onesho hilo la Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone.
Nyuma ya jukwa mwana dada Luren akipata flash ya pikee kabla ya unyesho kuanzaa



Wapenzi wa tazamaji wakisubiri kwa hamu onyesho hilo kuazarasmi ndani ya ukumbi wa Rendezvous mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S
Mwana muziki wa kizazi kimpya kwa muziki wa R&B ndani ya Washington DC, AJ Ubao akiwarusha vibaya sana wapenzi wa muziki wa nyumbani wanaoishi hapa DMV Jana jumatano Nov 23, 2011 Nchini Marekani.
Friday, November 25, 2011




Track mpya ya Diamond Platnumz inakwenda kwa jina “Mawazo” imefanyika AM Records, chini ya producer Maneke, inapatikana ndani ya album mpya ya Diamond inayoitwa “LALA SALAMA”, album ina nyimbo kumi ambazo ni 1.Moyo Wangu 
2.Lala salama
3.Chanda chema 
4.Nimpende nani 
5.Najua
6.Mawazo
7.Kwanini 
8.Gongolamboto 
9.Natamani 
10.Kizaizai
Thursday, November 24, 2011
Wednesday, November 23, 2011
                                                              TigerEyes

Mwanadada TigerEyes toka Arachuga anawaasa madem wote wanaofanya game wakaze buti mana yuko tight zaidi maelezo yani no mboyoyo hapa,"hakuna kulaza damu wala kusoundisha raia,niko serious sana na mziki chalaangu" asema nemy a.k.a TigerEyes mwanadafada anaye rap,kuimba na kudance katika crew la "NewKings" toka Arusha..."Noizmekah kwa dx ndo niliporekodia ngoma yangu hii ya "Grind on", beat ameunda producer Mosco ambae ameunda beat na vocal kasmamia bro dx mpaka ngoma kukamilika na kuwafikia wadau ma mashabiki zangu wote tanzania na dunia nzima,Sasa nakarbia kumaliza masomo ya chuo so nitakua full full hewani mithili ya noizmekah.com..Heshima tele ziende kwa Mungu kuniweka hai na my Mama kwa kunisuport katika muzik plus maproducer wangu kwa kuni guide na kunishauri...
Tuesday, November 22, 2011





Sshhhh,classic classic.. 
Keeping the good music alive, 
That’s me job, 
You my sunshine my moonlight and everything I dream about, 
Linah,let’s go..


Chorus.. 


Yalaiti,napenda pasi kifani/
Tofauti,sikutilii moyoni/ 
Sikuachi,leo na kesho peponi/ 
Anh anh anh anh anh anh I love you/ 


Verse I


Sambaza love kama dawa/
huachi mpaka napagawa/ 
hata ukisema mi sio Hamis natingisha kichwa/
mapenzi yako yanielemea ka chupa nzima ya tequila/ 
usirushe somo nakupenda acha masihara/ 
ina haja gani unishikie fimbo ili nikuskize ka gorilla/ 
mi ni mtu na mapenzi yangu nishaacha zamani usela/
una matatizo najua,na mi nna yangu boo/
we sit together from this moment,we see them through/
nikikukosea nisute,nipige vibao,nizodoe/ 
ninunie kwa siku kadhaa ila nnachoomba usinikimbie/
mapenzi ya utemi kwangu hadithi mambo ya kizamani hayo/ 
ukiniudhi ntapiga kwa khanga ndio nimefunzwa hivyo/
utaoga mabusu nikufute kwa kumbatio/
mpaka kama nikisafiri ukinikumbuka iwe kilio/
sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe/
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe/B… 


Chorus.. 


Verse II 


Nshasema sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe/
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe/ 
ushaangaliwa niunge tela usingoje mpaka uambiwe/ 
ushaangukiwa anguka nawe usizubae mpaka irejewe/ 
kwako ntakuwa Bushoke sitajiuliza ka zezeta/ 
yetu yawe mahaba mapenzi zamani tumepita/ 
mi sakafuni we ukingoni mbio zangu haziendi mbali/ 
una moyo wangu ntapenda bila kujali/
hata marefa wana timu zao mama panga matokeo/ 
pambano lianze najua goli ngapi ngapi leo/ 
usiache kuvaa nguo ndefu hivi vimini achia vicheche/ 
mwanamke kwetu staha tunaovipenda sio wote/ 
akili haziuwezi moyo na wenyewe una ubongo pia/
hauwezi ukafuatafuata kila utakachouambia/
nitajiwapo mapenzi naipata picha yako kwanza/ 
natamani uipate yangu na iwe inakuliwaza/


Linah..


Toa shaka na wasiwasi moyoni/ 
Toa shaka na wasiwasi moyoni/
Kukuepuka hilo haliwezekani/
Takushika,leo na kesho peponi/
Monday, November 21, 2011
THE CRUISE BEACH PARTY,THE ONE & ONLY HOTTEST BEACH PARTY IN TOWN; VENUE; MBALAMWEZI BEACH CLUB 
DATE; THIS SATURDAY 
TIME; 9 PM 
ENTREE; 10,000 TSH 
FREE COCKTAIL TO FIRST 200 PEOPLE


                  Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kulia) Joseph Mbilinyi a.k.a Mr, SUGU akionyesha kitabu ambacho ameelezea maisha yake kitakachopatikana wakati wa Shoo ijulikanayo Anti Virus katika Tamasha la Burudani kwa washabiki2011 litaakalofanyika Nov. 26,2011 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo, (kushoto) ni Msanii Fred Malaki a.k.a. MKOLONI. ( _Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO,)



            Waziri kivuli wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Joseph Mbilinyi (a.k.a. MR. SUGU -alievalia kadeti) leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 21-nov-2011 kuhusu shoo ijulikanyo Anti Virus wakati wa Tamasha la Burudani kwa washabiki 2011-i litalaofanyika jijini DSM hapo Nov. 26 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi,(kushoto) ni Msanii Fred Malaki (a,k,a- MKOLONI) n a Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a ZAY –B, Katika tamasha hilo Wasanii mbalimbali watatumbuiza, -Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO,



            Msanii Suma g akiimba mbele ya wana habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo. 

Mheshimiwa Nchimbi mgeni rasmi uzinduzi wa Albamu ya Anti Virus 2

 Gradice Siger
 Maelezo
  Dar es Salaam
            Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Emanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya wanamuziki wa kizazi kipya inayoitwa Anti Virus 2.
         Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam mratibu wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi alisema uzinduzi wa albamu hiyo unalengo la kuwakomboa vijana waweze kunufaika na kazi zao.
                 Mheshimiwa Mbilinyi amesema kwa muda mrefu wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakizulumiwa na wajanja wachache kitu ambacho kimewaacha wasanii hao kuendelea kuwa maskini. 
"Kuna wajanja wachache ambao kwa muda wa miaka mingi wamekuwa wakinufaika na jasho la wasanii sasa tumeamua kufanya mapinduzi kwa kuwaungunisha wasanii ili waweze kutetea haki zao".Alisema Mheshimiwa Mbilinyi. 
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii tarehe 26 Novemba kuanzia saa 12-6 usiku ambapo jumla ya wasanii zaidi ya 20 watashiriki ikiwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge na mawaziri ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 5000. Katika tamasha hilo Mheshimiwa Mbilinyi atauza kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake ambacho kitauzwa kwa shilingi 5000.
Saturday, November 19, 2011
Bila shaka yaelekea huu ni msimu mpya wa ngoma mpya kuachiwa.Kila msanii anataka kufurahia mwisho wa mwaka akiwa ameachia kitu kipya hewani.Huenda hiyo ndio zawadi ya Xmas kwa mashabiki. 

Mambo kadhaa yamemtokea Marlaw mwaka huu.Kikubwa zaidi ni kwamba hivi sasa ni mume wa mtu.Utakumbuka kwamba yeye na msanii mwingine,Besta,walifunga ndoa mwaka huu katika mojawapo ya harusi ambazo ziligubikwa na usiri mkubwa hususani kwa upande wa vyombo vya habari.Baada ya ndoa akawa kimya kidogo katika masuala ya muziki hususani kwa upande wa kutoa vibao vipya ingawa amekuwa akionekana majukwaani hususani katika shughuli mbalimbali zinazohusu Chama Cha Mapinduzi.Marlaw ni mtu asiyeficha mapenzi yake kwa chama tawala. 

Sasa baada ya kutamba na vibao kadhaa kikiwemo kile cha Pii,Pii(Missing My Baby),msanii Marlaw(ukipenda unaweza kumuita mume wa Besta) ameachia kibao Mbayuwayu(Ngo ngo ngo).Bila shaka hii itakuwa ni another sing-a-along kutoka kwa Marlaw.Ni utabiri wangu wa haraka haraka.Wimbo huu umetengenezwa pale Fishcrab chini ya Producers Lamar,Tud Thomas na Dunga.Usikilize hapo chini Read more: BongoCelebrity
Monday, November 14, 2011
Tamasha kubwa la Str8 Music limefanyika mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo kama anavyoonekana msanii Nameless kutoka Nchini Kenya akifanya Show kali iliyowavutia Wadau wengi kwenye Tamasha la STR8 MUZIK Inter College Special katika Viwanja vya Royal Village na kuhudhuriwa na wapenzi kibao wa muziki. PICHA ZOTE NA JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG
Msanii Barnaba akifanya show katika tamsha la STR8 MUZIK INTER COLLEGE SPECIAL 2011 katika Viwanja vya Royal Village
Walimbwende wakiserebuka ngoma za Juma Nature aka Kibra wakati alipopanda jukwaani
Mashabiki wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Royal Village mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo
Baada ya vichwa vya magazeti kadhaa ya bongo kuandika kwamba BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA) limetangaza kuufungia wimbo wa HAKUNAGA wa SUMALEE, katibu mkuu wa Baraza hilo amezungumza katika EXCLUSIVE na millardayo.com

 Gonche Materego amesema baraza hilo mpaka sasa hivi HALIJAUFUNGIA wimbo huo, lakini limekua na majadiliano makubwa kuhusiana na nyimbo nyingi za wasanii wa Tanzania ambazo tungo zake ZINAHARIBU lugha ya kiswahili ambapo HAKUNAGA ndio uliozungumziwa sana kama MFANO kwa sababu kiswahili kilichotumika ndani yake SIO SAHIHI.

 Materego amesema wimbo huo ulizungumziwa saaaaana, na hata watu wengine wa kawaida ambao hawafanyi kazi na BASATA walisema kwamba UNAPOTOSHA KISWAHILI na kwa vile wasanii ni walimu wakuu wa kiswahili ni rahisi sana watu wa kawaida kutumia lugha za wasanii wakidhani kuwa ni sahihi lakini sio.

 “wenzetu wa baraza la kiswahili wameona kuna haja ya kukaa na kujadiliana kuhusiana na tatizo la kiswahili kuharibiwa kwenye nyimbo za wasanii, tutakutana na wasanii tusikie wanachokisema na wananchi pia wasiki ili tupate michango mizuri zaidi kabla hatujakaa BASATA na BAKITA kuandaa mipango zaidi” ameamplfy Materego. hiyo ndio story kutoka BASATA na BAKITA! nipe maoni yako kuhusiana na unachofikiria………?! Habari na millardayo.com
Friday, November 11, 2011
Album mpya ya msanii mkali wa bongo flava anayefahamika kama Diamond Platnumz sasa ipo madukani nchini kote. Album inakwenda kwa jina “Lala Salama” ikiwa imebeba nyimbo kali kama vile “Moyo Wangu”, ngoma inayoendelea kufanya vizuri kwenye chati mbambali. Jipatie nakala yako sasa!!
Thursday, November 10, 2011
BODA KWA BODA BEACH CONCERT ON 12th Nov.....,here comes what you have been waiting for tz BODA KWA BODA BEACH CONCERT..Stage will be covered by Jaguar from Kenya ,Sumalee,Country boy & Stamina,GodZilla,Aslay,Beka,Reycho,Young D and many more.Dj Zero will be on the mix to make the crowd going crazzieeee with the hottest hitz. ENTRANCE : 10,000tshs VENUE: MBALAMWEZI BEACH "the finest beach" TIME: 7pm Proudly brought to you by G5 CLICK.....
Wednesday, November 9, 2011
SQUIZER ft. OMMY DIMPLE - BACHELLAR
Brand New Song kutoka kwa MwanaFA akiwa amemshirikisha Linah, YALAITI ambao umefanyiwa sample kutoka kwa wasanii wakongwe ambao waliutumia toka kitambo, hapa namzungumzia Siti, Binti Saad, Malika pamoja na Bibi Kidude. Wimbo huu kwenye chorus ameimba Linah na kurudia kwa melody ile ile halafu mtu mzima akadondokea. Gitaa limepigwa na mmoja wa walimu wa muziki THT anaitwa Cadinal Gento na beat imefanywa na Marco Chali kutoka MJ Rec Isikilize YALAITI Hapa
Friday, November 4, 2011
Hello mdau..attached is my new track called ME WA KITAA produced by Levyzbeatz at UrbanAksent records in Uganda...nitakushkuru tukifkishia huyu na yule so we an all enjoy the music.. pamoja sanaaa ITS YOUNG SUMA.
Wednesday, November 2, 2011
Tuesday, November 1, 2011

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Blog Archive

CONTACT US

Lukata Willy,
BK,
Houston TX,
U.S.A

Tel:
832-859-6047
E-Mail:
lukatawilly@ymail.com
http://angrybirdsgamer.com

Total Pageviews

NEW EAST AFRICA SONG



Lukata Willy

Lukata Willy
ITS NOT WHAT YOU HAVE IN YOUR LIVE, BUT WHO YOU HAVE IN YOUR LIFE THAT COUNTS

FOLLOWER US ON

BONGOFLAVA

Like Us on Facebook

COUNTRY VISIT MY WEB

Home

Create by Bongotrack. Powered by Blogger.

BLOG FANS